Tanzania kuboresha mazingira ya uwekezaji
DAR ES SALAAM :WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji na wafanyabiashara kuhakikisha wanapata manufaa makubwa kwenye uwekezaji wao wenye manufaa na tija kwa maslahi mapana ya Taifa.
Akizindua taarifa taarifa ya maboresho ya mazingira ya uwekezaji na biashara na nyenzo za usimamizi wa uwekezaji nchini jijini Dar-es-salaam, Waziri Mkuu amesema serikali inaendelea kuboresha mifumo ya tehama ili kuwahudumia wawekezaji na wafanyabiashara unaoitwa (Tanzania Electronic Window) ili kumwezesha mwekezaji kusajiri mradi wake ndani ya nchi lakini pia akiwa nje ya nchi na kupata vibali vya uwekezaji ndani ya mda mfupi wamekadiria iwe siku tatu.
Aidha Majaliwa amesema kuwa nchi ya Tanzania ina usalama kwa uwekezaji na biashara huku akiweka msisitizo kwa Ofisi ya Rais, Mipango na uwekezaji kuwa Taasisi na mamlaka ya serikali za mitaa ziharakishe marekebisho ya taratibu na sheria zinazochangia urahisi wa kufanya biashara , Taasisi zote za Umma na mamlaka ya serikali za mitaa waogeze ushirikiano wa karibu na sekta binafsi naTaasisi zote zinazoshughulikia uwekezaji na biashara ziwekeze kwenye mifumo ya kieletroniki na mawasiliano ili kuboresha usimamizi wake.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais , Mipango na uwekezaji Prof.Kitila Mkumbo amesema katika kipindi cha mwaka mmoja waliandaa na waliwasilisha Bungeni muswada wa uwekezaji wa Umma wa mwaka 2023 ambao ushasomwa mara ya kwanza na wanatarajia bunge lijalo watasoma mara ya pili na Ofisi imeshaandaa rasimu ya sera mpya ya uwekezaji nchini ya mwaka 2024 itakayochukua nafasi ya sera ya uwekezaji ya mwaka 1996.
Kitila amesema Juni mwaka 2019 serikali ilizindua mpango kazi wa utekelezaji wa mpango wa kuboresha mazingira ya wafanyabiashara (MKUMBI) wenye lengo la kufanya uchambuzi wa mazingira ya wafanyabiashara nchini na kuainisha mageuzi na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika kutatua changamoto za kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na uwekezaji.
SOMA : Iringa yavuta uwekezaji wa tril 20/-
Nae Mwenyekiti wa Sekta binafsi Raphael Maganga amesema serikali imefanya jitihada kubwa kuboresha mazingira ya wafanyabiashara nchini huku akiiomba serikali kuwa na sera ambazo hazibadiliki badiliki ziwe sera zinazotabirika , kusiwepo na sera zinazoathiri sekta nyingine na kuendelea kurudisha imani hasa katika sekta za mabenki.
Uzinduzi huo umeongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Naibu Waziri Mkuu,na Waziri wa Nishati , Dk. Doto Biteko na Kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Dk. Tausi Kida, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila pamoja na Viongozi mbalimbali.