Serikali yaahidi raha sekta ya mawasiliano

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesisitiza nia ya Serikali kuunga mkono uwekezaji wa sekta binafsi hasa katika sekta ya mawasiliano.

Waziri Nape ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya ujenzi wa minara ya mawasiliano kati ya kampuni ya Towerco of Africa Tanzania na British International Investment. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri Nape ameelezea kuwa ujio wa sekta binafsi katika uwekezaji wa mawasiliano ni matokeo ya kupitishwa kwa bajeti ya Serikali, na hivyo anaona ni mafanikio makubwa.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye

Amezipongeza kampuni hizo mbili kwa makubaliano yao na ametambua kuwa yataongeza nguvu katika harakati za mapinduzi ya nne ya viwanda nchini Tanzania.

Soma pia: https://habarileo.co.tz/mnara-mrefu-afrika-kujengwa-tanzania/

Ameihakikishia sekta binafsi kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji, ili kuchochea ukuaji wa sekta ya mawasiliano na kukuza uchumi wa nchi.

Soma pia: https://www.tiktok.com/@dailynewsdigital/video/7369144507369049350

#SmartTanzania #TzyaKidijitali #KaziIendelee

Habari Zifananazo

Back to top button