Serikali yaeleza hali ya usalama mpaka wa DRC

DODOMA; SERIKALI imesema hali ya usalama ya mpaka wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wenye urefu wa kilometa 554 ni shwari.

Hata hivyo, imesema mpaka huo unakabiliwa na changamoto za kiusalama kutokana na mapigano yanayoendelea mashariki mwa DRC kati ya jeshi la nchi hiyo na makundi yenye silaha, hususan Kundi la M23 na kwamba hali hiyo inaathiri usalama wa mpaka.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Mei 19, 2026 na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Rhimo Nyansaho akiwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

“Kundi la M23 linashikilia miji mbalimbali ya kimkakati katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini ikiwemo Goma na Bukavu na kudhibiti Mji wa Uvira.

“Kushikiliwa kwa miji hiyo kunaongeza changamoto za kiusalama katika mpaka huu. Aidha, juhudi mbalimbali za kikanda na kimataifa zimeendelea kuchukuliwa kurejesha amani ya kudumu nchini DRC.

“Wizara kupitia JWTZ, imeendelea kufuatilia hali hiyo kwa ukaribu ikiwemo kufanya doria mara kwa mara katika mpaka huu,”amesema Waziri wa Ulinzi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button