Serikali yaipongeza NMB mkopo bil 100/- nishati safi

SERIKALI imeipongeza Benki ya NMB kwa kuzindua Mfuko Maalu[1]mu uliotengewa Sh bilioni 100 za kukopesha wasambazaji na wauzaji wa nishati safi ya kupikia kwa Watanzania.

Imesema itaingia kifua mbele katika Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika (Mission 300), unaoanza leo hadi kesho Dar es Salaam.

Pongezi hizo zilitolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko, wakati wa uzinduzi wa mfuko huo, aliobeba dhamira chanya ya kuunga mkono juhudi za serikali katika Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034) na kwamba tukio hilo ni uthibitisho tosha wa ushirikiano uliopo baina ya serikali na sekta binafsi kustawisha jamii ya Watanzania.

Advertisement

Kwa niaba ya serikali na Wizara ya Nishati, Dk Biteko aliishukuru NMB kwa wazo hilo na kwamba wako tayari kuwaunga mkono ili jambo hilo likatimizwe, huku akisema wazo la kuhakikisha mawakala na wasambazaji wa nishati safi za kupikia wanapata mitaji ili kufikisha huduma mijini na vijijini, litasaidia kuchochea upati[1]kanaji na matumizi ya nishati hiyo.

“Hakika mpango huu wa NMB kutenga Shilingi bilioni 100 kwa ajili ya jambo hili, unastahili pongezi kubwa sana hasa ikizingatiwa kuwa kama benki ina njia nyingi sana za biashara, ambazo wangeweza kuwekeza fedha hizo sehemu nyingine ili kuweza kuendelea kujizal[1]ishia faida zaidi,” alisema Dr Biteko.

“Lakini, msukumo huu wa kuja kuweka kiasi hiki kwenye nishati safi ya kupikia inaonesha dhamira ya dhati ya benki kuchangia maendeleo endelevu kwa taifa letu la Tanzania, lakini ni kielelezo tosha cha uza[1]lendo wa kweli uliopo kati yenu Menejimenti pamoja na wafanyakazi wa benki hii,” aliendelea.

“Mtendaji Mkuu wa NMB tayari ameeleza hapa faida mbalimbali za matumizi ya nishati safi ya kupikia na mimi nisisitize kuwa, faida hizo za afya bora, mazingira safi, kuboresha uchumi na ufanisi wa nishati hizi na ukweli kuwa nishati safi ni salama, ndio maana hata Rais Samia Suluhu Hassan ame[1]kuwa kinara wa hili nchini, Afrika na duniani kote,” alisema.

Aliongeza: “Wote tunafahamu kwamba, licha ya ukosefu wa mitaji, changa[1]moto kubwa ya wananchi kuendelea kutumia nishati isiyo safi ya kupikia, ni ukosefu wa elimu juu ya nishati safi ya kupikia, hivyo suala la NMB kuanza pia kutoa elimu ya hili ni jambo zuri na la kipekee sana kwa ustawi wa matumizi ya nishati hii safi”.

Alisema shukrani na pongezi kwa NMB hazi[1]taishia tu katika nishati safi ya kupikia tu, bali zinaenda pia kwa mambo makubwa ambayo imekuwa ikifanya kwa manufaa kwa taifa, ikiwemo misaada mbalimbali mashuleni, zahanati, vituo vya afya na hospitali na ku[1]chagiza maendeleo endelevu kwa jamii, sambamba na upandaji miti.

Awali, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema msukumo wa benki yake kutenga kiasi hicho kikubwa cha pesa za kukopesha wafanyabiashara na wasambazaji wa nishati, unalenga kuwezesha utunzaji wa mazingira, kuboresha afya na ustawi wa jamii, kukuza uchumi na kuchangia kufikiwa kwa Malengo Ende[1]levu ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2030.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Zaipuna alisema lengo ni kuongeza urahisi katika upatikanaji wa nishati safi kwa Watanzania na kwamba, NMB inatambua umuhimu wa kuungana na serikali kufanikisha Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati nafuu, kwa urahisi, endelevu na ya kisasa kwa wote.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *