Serikali yalipa deni trilioni 4/- PSSSF

SERIKALI imelipa madeni ya zaidi ya Sh trilioni 4.27 za watumishi yaliyokuwa yanadaiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Fortunatus Magambo alisema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa sekta ya kinga ya jamii jijini Arusha.

Magambo alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia ulipaji wa madeni ya michango ya watumishi ambayo mfuko huo ulikuwa ukidai kwenye taasisi mbalimbali.

SOMA: PSSSF waja kisasa zaidi mafao ya wastaafu

Alisema PSSSF kwa sasa ina thamani ya zaidi ya Sh trilioni 13 na inakusanya Sh trilioni tatu za michango ya wanachama kila mwaka.

“Tunaendelea vizuri, mfuko upo salama, wanachama wetu msiwe na wasiwasi, tunawekeza kwenye maeneo mbalimbali ambayo yanasaidia kukuza uchumi na kuongeza ajira kwa Watanzania,” alisema Magambo.

PSSSF ilianzishwa Agosti Mosi, 2018 na kupewa jukumu la kusimamia michango ya watumishi wa umma kwa ajili ya akiba ya kustaafu na kulipa mafao ya wastaafu.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu alisema hadi sasa serikali imelipa asilimia 95 ya deni ambalo lilirithiwa kutoka kipindi cha kabla ya mwaka 1999.

Sangu alisema kulipwa kwa madeni hayo kumeongeza kasi ya ulipaji wa mafao kwa wakati na kuleta utulivu wa kiuchumi kwa wastaafu

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com

  2. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button