Serikali yaonya utapeli misaada Kariakoo

DAR ES SALAAM – Serikali imesisitiza kuwa michango na misaada yoyote kwa ajili ya kusaidia waathirika wa kuporomoka kwa jengo Kariakoo jijini Dar es Salaam itafanywa kupitia akaunti maalumu ya maafa 9921159801 ambayo ipo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dk Jim Yonazi amewaambia wanahabari kuwa nnamba hiyo ndiyo itakayohusika kupokea msaada wa kifedha kutoka kwa wasamalia wema.

“Kuna watu wana nia njema kabisa kwaajili ya kuwasaidia Watanzania, lakini naomba tujizuie kabisa kukusanya michango ya kifedha kutoka kwa mtu yeyote bila kupitia akaunti hii,” amesema Dk. Yonazi.

Advertisement

Aidha amesema akaunti hiyo ni maalumu imethibitishwa na serikali ili kuweza kuhakikisha misaada inawafikia walengwa na inatimiza malengo ya kutoa misaada hiyo.

Amesema kwa sasa operesheni inaendelea mpaka pale watakapokamilisha zoezi la kuokoa watu ambao bado hawajaokolewa.