Serikali yapanga kuongeza ndege kuchochea uchumi

CAPE TOWN: SERIKALI imetangaza mpango wa kuongeza ndege nane kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), hatua itakayofikisha jumla ya ndege 24 ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usafiri wa anga na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Taarifa hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, alipokuwa akizungumza na watumishi wa ATCL katika miji ya Cape Town na Johannesburg nchini Afrika Kusini, ambapo ameelezea kuwa shirika hilo lilianza na ndege moja mwaka 2016 na sasa lina ndege 16

Aidha, katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, serikali imeongeza ndege sita kubwa, kwa lengo la muda mfupi ni kufikia ndege 19 ndani ya mwaka wa fedha 2025/2026, kabla ya kufikia ndege 24 ifikapo mwaka 2030.

Ongezeko hilo la ndege limewezesha kupanuka kwa mtandao wa safari za ndani, ambapo kwa sasa ATCL inahudumia miji mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Mtwara, Kigoma, Iringa, Pemba, Unguja, Songea, Mpanda, Tabora na Bukoba. Aidha, mipango ipo ya kuanza safari katika miji ya Sumbawanga, Musoma na Shinyanga hivi karibuni.

Katika ngazi ya kimataifa na kikanda, shirika hilo linaendesha safari zake katika miji ya Nairobi, Entebbe, Bujumbura, Lubumbashi, Lusaka, Harare, Johannesburg, Guangzhou (China), Mumbai (India) na Dubai, pamoja na huduma za usafirishaji mizigo (cargo) zinazochangia kukuza biashara na uchumi wa taifa.

Katika hotuba yake, Kihenzile amewahimiza watumishi wa ATCL kuendelea kufanya kazi kwa weledi, nidhamu na uwajibikaji kwa manufaa ya taifa.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana, amebainisha kuwa uwepo wa ATCL katika miji ya Johannesburg na Cape Town unachochea ukuaji wa biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button