DAR-ES-SALAAM : KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeshauri serikali kujenga majengo maalumu kwa maafisa ustawi na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili kuboresha malezi bora kwa watoto.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Riziki Said, alisema wazazi wanapaswa kujua majukumu yao ili kupunguza idadi ya watoto wa mitaani.
Ushauri huu umetolewa baada ya kamati kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ukumbi wa Mihadhara wa Chuo cha Ustawi wa Jamii. SOMA: Serikali kuimarisha huduma ustawi wa jamii
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mwanaid Khamis, alisema maendeleo ya jengo hilo ni mazuri na litatoa mazingira rafiki kwa wanafunzi.
Dk. Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, alisema wataboresha huduma za kijamii kwa maafisa ustawi. Msanifu wa Majengo, Dickson Mark, alieleza kuwa mradi umefikia asilimia 35, na utamalizika Juni 22, 2025.
Mkuu wa Chuo cha Ustawi, Dk. Joyce Nyoni, alieleza changamoto za mradi, ikiwemo mtililiko dhaifu wa fedha, lakini alisisitiza umuhimu wa mradi huo kwa kuongeza idadi ya madarasa. Mradi huu unajengwa kwa mapato ya chuo na utatoa huduma kwa watu 400.
Kituo cha Taifa cha Kulelea cha Kurasani ni miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa na kamati hiyo.
buy viagra online
Can you imagine making $18,000 a month while working from home just a few hours a day? I’m doing it, and I never thought it was possible until I found this online opportunity. The work is super easy, and you don’t need any prior experience—just a desire to succeed! I can’t believe how much my life has changed in such a short time. If you’re ready to take control of your income, visit the website and get started today!
Visit This…… Www.EarnApp1.Com