Serikali yataka TRA kuheshimu sheria

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande, ameitaka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuheshimu sheria ya kodi na fedha na kuhakikisha wajasiriamali wote wanaoanza kufanya biashara nchini hawalazimiki kulipa kodi kwa kipindi cha angalau miezi sita kwa mujibu wa sheria ya fedha ya mwaka 2019.

Chande amemwagiza Kamishina Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata kuhakikisha sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge inatekelezwa na kwamba mjasiriamali mpya hatozwi kodi baada ya kuanza kufanya biashara.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Ng’wasi Damas Kamani, Naibu Waziri amesema pia Serikali itafanya mapitio ya Sheria ya Uwekezaji na ile ya Fedha ya mwaka 2019 kuongeza muda wa kodi kwa wawekezaji wazawa.

Katika swali lake, Mbunge alihoji ni lini serikali itafanya mapitio ya sheria hiyo ili kuongeza muda wa kodi kwa wazawa kwa muda wa kati ya miezi 12 hadi 18 ili  kutoa motisha kwa wawekezaji wa ndani na kuwaongezea fursa ya ushindani na wawekezaji wa nje ambao sheria inawapa ruhusa ya msamaha wa kodi wa hadi miaka 5.

Awali, Kamani alihoji ni kwa nini serikali imeendelea kutoza kodi wafanyabiashara wapya kwa mgongo wa kibali cha kodi ‘tax clearance’ ingawa sheria ya fedha ya mwaka 2019 inatoa nafuu kwa mjasiriamali kupata ahueni ya kutolipa kodi kwa miezi 6 baada ya kuanza kufanya biashara.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x