Serikali yatangaza Neema kwa Wanawake
Sasa washindwe wenyewe

DAR ES SALAAM: SERIKALI imesema itaendelea kuwainua wanawake kwenye sekta mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi kufikia maendeleo.
Hayo yamesemwa, Jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa, alipokuwa akimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji katika mkutano wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali yenye lengo la kuwainua wanawake nchini Womeni Creating Wealth (WCW).
“Kumwezesha mwanamke ni kuisaidia jamii ili kuweza kukuza uchumi wake na kufikia malengo,”amesema Nyaisa.
Hata Hivyo, Nyaisa amewataka wanawake nchini wenye nia ya kuinua biashara na kujiepusha na matapeli ni wakati sahihi kujisajili na kusajili biashara zao BRELA ili kuepukana na utapeli.
“BRELA ni taasisi ya kukuza biashara, na tunawataka wanawake wote kusajili biashara zao hapa,na kujiepuka na kutapeliwa”ameongeza.
Pia Nyaisa ametumia mkutano huo kuwataka wanawake hao kuhakikisha wanakuwa na banda lao la kuonesha kazi zao za ujasiriamali kupitia maonesho mbalimbali ili kuwainua wanawake wengine.
Kwa upande wake Meneja wa WCW,Anabahati Mnale, amesema taasisi hiyo imefanikiwa kuwainua wanawake mbalimbali na kuwajengea kiuchumi
“Tumewajengea wanawake mbalimbali kiuchumi toka 2016 wanawake wamekuwa wakinufaika”amesema
Kwa upande wake, Mosi Hassai ambaye ni mjasiriamali ameishukuru WCW kwa hatua yake ya kuwainua wanawake nchini na kuwapa mafunzo ya kuchungulia fursa.
“Tangu nimejiunga nimejifunza na nimepata fursa za masoko ya ndani na nje,nawashukuru sana elimu hii itawasaidia na wanawake wengine kufika mbali kibiashara”amesema
Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by follow instructions….
.
.
.
On This Website……………..> > http://remarkableincome09.blogspot.com