DAR ES SALAAM: SERIKALI imefanya maboresho 605 ya kisera, kisheria, kikanuni katika kipindi cha miaka mitano iliyopita 2019 hadi 2023 ili kuvutia wawekezaji
Hayo yamesemwa leo Februari 27, 2024 na Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo jijini Dar es Salaam katika Jukwaa la Kodi na Uwekezaji.
Amesema, maboresho 416 sawa na asimilia 64 yalilenga kuweka mazingira bora ya biashara na uwekezaji nchini.
Pia, maboresha 460 kati ya maboresha 665 yamefanyika kati ya mwaka 2022- 2023 sawa na asilimia asilimia 70.
Prof Kitila amesema maboresho hayo yamefanyika ili kuvutia wawekezaji ambao wamekuwa wakiangalia utulivu wa kisiasa na amani katika nchi husika, mazingira ya kisheria hususani kwenye ulinzi wa mali mwekezaji atawekeza kwenye nchi husika.
“Tumeweka mazingira mazuri ya kisheria, kuhakikisha mali zao zinakuwa salama, uwepo wa soko kwa bidhaa watakazozalisha,”amesema Prof Kitila.
Amesema, soko la Tanzania ni kubwa na inakadiriwa miaka 10 ijayo itakuwa miongoni mwa nchi nne zenye idadi ya watu ni wengi.
“Tanzania ni lango kuu la soko ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) tunazungumzia idadi ya soko ya watu milioni 400.
“Lakini pia tumejiunga na soko la Jumuiya ya Biashara Afrika (CFGA) yenye takribani ya watu bilioni moja,”amesema.
Aidha, amesema pia utulivu wa kiuchumi na utulivu wa fedha kwa ujumla. Uwepo wa vipajji na nguvu kazi, ubora wa miondombinu ni chanzo kingine cha kuvutia wawekezaji.
“Kodi, viwango vya chini inajitokeza kuwa ni namba saba kuvutia wawekezaji, gharama ndogo za nguvu kazi, uwepo wa ardhi na uwepo wa fedha na kugharamia miradi ya uwekezaji,”