Serikali Yawataka Wasanii Kurejesha Mikopo

DAR ES SALAAM: Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amewataka wasanii wa sanaa nchini  kurejesha mikopo waliyopewa na mfuko wa utamaduni na sanaa Tanzania.

Akizungumza na wasanii wa sanaa jijini Dar-es-salaam, Mwinjuma amesema lengo la serikali kuwapa wasanii fedha hizo ni kutaka kuwasaidia kuboresha kazi zao za sanaa.

“mikopo hiyo sio ruzuku bali ni mikopo inayopaswa kurejeshwa,” amesema.

Advertisement

SOMA: Dk Mapana awaita wasanii BASATA

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Utamaduni wa Sanaa Nyakaho Mahemba amesema serikali imetoa shilingi Bilioni Tatu kutoka Bilioni 1.6

“ tunataka kuona lengo la kaunzishwa mfuko huo liendelee”alisema  Mahemba

Naye Rais wa Shirikisho la Filamu nchini Rajab Amir  amesema changamoto kubwa ni masharti kwahiyo ametoa ombi kwa serikali kupunguza masharti hayo ili walengwa waweze kunufaika na mfuko huo.