Serikali yaweka mkakati kuinua zao la mchikichi

SERIKALI kupitia Wizara ya kilimo imeeleza mkakati wake wa kuboresha miundombinu ya kituo cha Utafiti cha TARI – KIHINGA kuwa cha kisasa kwa kuwa na miundombinu bora na kuongeza uzalishaji wa miche ya michikichi.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde, katika ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani Kigoma ya kutathmini zao la mchikichi.

Amesema ili kutekeleza mpango wa uzalishaji bora wa mbegu za Michikichi uweze kueleta matokeo bora na makubwa zaidi, katika bajeti inayokuja, serikali imetenga fedha kwajili ya kuboresha miundombinu ya kituo hicho cha Utafiti cha TARI – KIHINGA.

Advertisement

Pamoja na hayo pia tumekipatia kituo hichi Sh bilioni 2.7 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi, maabara na nyumba za watumishi.”Amesema Mavunde

Amesema pia Wizara ina mpango wa kuwajengea uwezo watafiti wa zao hilo la mchikichi kwa kuwapeleka masomoni na kujifunza katika maeneo ambayo yamefanya vizuri zaidi.

Mavunde amesema katika kuzijengea uwezo taasisi zinazo husika na uzalishaji wa Miche ya Michikichi pamoja na kuboresha usimamizi wa uzalishaji huo, Wizara yake inashauri fedha zinazotengwa na halmashauri kwa jili ya usimamizi wa Miche ya michikichi, zielekezwe pia kwenye taasisi kubwa zinazo zalisha Miche ya Michikichi, Taasisi hizo ni kama vile, JKT Bulombora, Gereza la Kwitanga pamoja na TARI, ili kuleta Tija.

Amesema uzalishaji wa miche bora aina ya TENERA utaenda sambamba na kuwaunganisha wakulima wadogo pamoja na vikundi vya wanawake na SIDO ili waweze kupata mitambo rahisi ya uchakataji wa mafuta ya mawese na kujiongezea kipato kupitia benki ya maendeleo ya kilimo (TADB)ambayo mpaka sasa imeidhinisha kiasi cha Sh 1,400,000,000 kwa ajili kuchochea shughuli za uongezaji thamani wa zao la mchikichi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema mwamko wa wananchi kulima zao la mchikichi ni mkubwa na mahitaji ya miche bora pia ni makubwa hivyo juhudi ya wizara ya kilimo ya kukiongezea uwezo kituo cha TARI-KIHINGA itakuwa ni hatua kubwa ya maendeleo ya zao la mchikichi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *