Sh bil 429/- zatekeleza miradi ya maji miaka 4 Kigoma

KIGOMA: MKOA wa Kigoma umepokea Sh bilioni 429 kutekelezaji  miradi ya maji kwa kipindi cha miaka minne ya Rais Samia madarakani.

Lengo ni kusogeza huduma ya maji karibu na makazi ya watu ili kuondoa usumbufu wa kutumia muda mwingi na kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigom, Thobias Andengenye amesema hayo wakati akizundua mradi wa maji katika kijiji cha Mtego wa Noti Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Amebainisha kuwa Serikali ya Rais Samia imedhamiria kuondoka kabisa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa Watazania.

Andengenye amesema kuwa dhamira ya dhati ya serikali kutumia fedha zake za makusanyo ya kodi na misaada ya wafadhili haitakuwa na maana kama miradi hiyo inashindwa kutekeleza malengo hayo kwa kuharibika muda mfupi baada ya kukamilika hivyo alitaka wananchi kuwa walinzi wa miradi hiyo iweze kudumu kwa muda mrefu sambamba na kuchangia gharama za uendeshaji.

Awali akitoa taarifa kuhusu mradi huo wa Mtego wa Noti Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)  Uvinza, Mhandisi Bakari Kiwitu amesem kuwa kiasi cha Sh bilioni 1 kimetumika katika utekelezaji wa mradi huo wenye lengo la kupeleka huduma kwa wakazi 9448 wa vijiji vya Mtego wa Noti na Mganza.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa UNICEF mkoa Kigoma, Justus Ndenzako alisema kuwa Shirika hilo limetoa fedha kiasi cha Sh milioni 952.6 kupitia mfuko wa Poul Due Jenson, Grundfos ikiwa ni sehemu ya Sh bilioni 9.2 ambazo Shirika ilo limechangia miradi ya maji mkoani Kigoma ambapo wananchi wa vijiji hivyo viwili wamechangia kiasi cha Sh milioni 47.6.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button