Sh Bil.718 zatumika kujenga vituo vya afya

DODOMA: KATIKA kipindi cha miaka mitatu serikali imejenga jumla ya vituo vya afya 466 vilivyogharimu Sh Bilioni 718.1.

Hayo yamesemwa leo Februari 15, 2024 na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dk Festo Dugange amesema ambapo amesema vituo hivyo vimejengwa katika mwaka wa fedha 2021/22, 2022/23 na 2023/24.

“Jumla ya vituo vya afya 466 vilivyogharimu Sh Bilioni 718.1 katika maeneo ya kimkakati kote nchini ambapo Mkoa wa Simiyu jumla ya vituo vya afya nane vimejengwa katika Kata za kimkakati kwa gharama ya Sh Bilioni nne,”amesema Dugange

Amesema, serikali itaendelea kutenga bajeti kwa awamu kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika Kata za kimkakati kote nchini zikiwemo kata katika Halmashauri za Mkoa wa Simiyu.

Habari Zifananazo

Back to top button