SERIKALI imetenga bajeti Sh bilioni 8.
75 kwa mwaka wa fedha 2023/2324 kwa ajili ya ujenzi, upanuzi na ukamilishaji wa vituo vya afya 20 katika halmashauri.
Hayo yamesemwa leo Aprili 4, 2023 na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Dkt Festo Dugange bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Biharamulo, Injinia Ezra Chiwelesa aliyehoji ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vituo vya afya vya Rukaragata, Kalenge na Nyabusozi na Biharamuro
Amesema vituo vya afya vya Rukaragata, Kalenge na Nyabusozi ni miongoni mwa vituo vya muda mrefu na miundombinu yake inahitaji maboresho kulingana na mahitaji ya sasa.
Pia, amesema Halmashauri ya Wilaya ya Biharamuro imetengewa sh milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa vituo vya afya viwili kati ya vitatu vyenye mahitaji.
Aidha, Dkt. Dugange amesema amesema utaratibu wa kutenge bajeti kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa vituo vya afya chakavu ni endelevu.