Sh bilioni 230 kuboresha miundombinu ya elimu ya awali

SERIKALi imetoa Sh bilioni 230 kuanza uboreshaji miundombinu ya elimu ya awali na elimu ya msingi ukiwemo ujenzi wa madarasa maalumu ya mfano kwenye shule 302 zinazojengwa katika halmashauri 184 kwa ajili ya kujifunzia wanafunzi wa elimu ya awali.

Mratibu wa Mradi wa Boost kutoka Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ,Ally Salehe alisema hayo  mjini Morogoro

Salehe alibainisha hayo wakati wa kumkaribisha Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk Lyabwene Mtahabwa  kwenye ufunguzi wa  mafunzo kwa wawezeshaji wa kitaifa kuhusu mafunzo ya walimu wanaofundisha wanafunzi wa elimu ya awali .

Advertisement

Mratibu wa Boost kutoka Tamisemi alisema kuwa ,katika bajeti yam waka 2022/2023 , serikali ya awamu  ya sita ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha sh bilioni 230.

Mradi wa Boost umetengewa kiasi cha sh trilioni 1.15 ambao ni ufadhili wa Benki ya Dunia ambazo zimeelekezwa katika sekta ya elimu kuboresha elimu ya awali na msingi.

Alisema mradi huo ni sehemu ya mpango wa lipa kulingana na matokeo katika Elimu ya Awali ya Pili (EPFORR II) na inachangia utekelezaji wa mpango wa Maendeleo ya Elimu wa miaka mitano 2021/22 hadi 2025/26.

Salehe alisema licha ya  kujengwa madarasa maalumu kwenye 302 katika halmashauri zote nchini, katika  shule za msingi ambazo zipo tayari  yatajengwa madarasa 368.

“ Madarasa haya miongoni mwa walimu wake ndiyo wanaojengewa  uwezo wa ufundishaji , na pia madarasa haya yatawekewa vifaa vilivyoboreshwa vya kuwawezesha wanafunzi wa elimu ya awali kujifunza kwa ufanisi” alisema Salehe

Alisema  mradi huo umekuja kwa ajili ya kutatua changamoto ambazo zipo katika  elimu ya awali na msingi , na moja wapo ni uwepo wa baadhi ya wanafunzi ambao wanapita darasa la kwanza na la pili bila  kumudu stadi za kusoma , kuandika na kuhesabu .

“ukiangalia kwenye mitihani ya taifa ya kumaliza elimu ya msingi bado haujafikia asilimia 100 , hivyo  mradi umelenga  kuboresha elimu ya awali na msingi kwenye  maeneo ya kuboresha mzingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule za mzingi za serikali “alisema Salehe

Alisema mradi  huo unalenga  kutatua  changamoto ili wanafunzi wote waweze kumudu stadi za kusoma , kuandika na kuhesabu iliwaweze  kupata stadi  au  umahili wa kuwawezesha wao kuendelea na elimu ya sekondari kuanzia kidato cha  kwanza hadi   kidato cha nne.

“ Hili ndilo lengo la taifa na ndiyo lengo la  mheshimiwa Rais la kuhakikisha wanafunzi wote , watoto wote wanaoanza elimu ya awali wanaweza kumaliza kidato cha nne, kuhakikisha ya kwamba  wanafunzi wote wa elimu ya awali wanaandikishwa kwenye madarasa ya elimu ya awali “ alisema Salehe

Naye  Katibu Mkuu wa Wizara ya  Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo, katika hotuba yake iliyosomwa na kamishna wa elimu wa wizara hiyo  Dk  Mtahabwa , alizitaka taasisi za umma ,kidini  kibinafsi binfasi , wazazi  na wadau wengine kuhakikisha wanaboresha  malezi na ukuzaji wa mtoto.

Alisema hatua hiyo ni pamoja na kuwekeza katika malezi , makuzi na madarasa  yanayoongea,  vyoo,  viwanja vya michezo ikiwa na kushirikiana na wadau kwa ajili ya kutoa chakula na lishe , afya , ulinzi na  usalama na michezo kwa watoto wote.

Profesa Nombo alitaja jambo lingine ni kuendelea kusajili vituo shikizi vya shule na kuwa shule kamili pamoja na kuwajengea uwezo wasaidizi wa walimu na wengine katika kutoa huduma jumuishi kwa maendeleo ya ujumla yam toto.

Hivyo aliwaomba  wadau wote wa Malezi , Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) , yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali na jamii kuendelea kushirikiana na serikali katika masuala ya malezi , makuzi na ujifunzaji wa watoto.

Profesa Nombo alisema hatua hiyo ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka kipaumbele katika sekta ya elimu ili kuhakikisha ya  kwamba watoto wote wanapata elimu inayokidhi viwango ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *