Sh bilioni 27 kuipendezesha Mikindani

SERIKALI imetoa zaidi ya Sh bilioni 27 fedha kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya mji Tanzania (TACTIC) katika Manispaa ya  Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara.

Hayo yamejiri leo Oktoba 10, 2025 wakati wa ghafla fupi ya utiliaji saini mkataba wa uboreshaji wa miundombinu ya mji Tanzania iliyofanyika kwenye manispaa hiyo.

 

Akizungumza wakati wa ghafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amemtaka mkandarasi anayetekeleza miradi hiyo kukamilisha miradi ndani ya wakati uliyopangwa ili wanan

chi waweze kupata huduma kwa wakati kwani hawatakuwa tayari kuona miradi hiyo ikichelewa.

“Ni matumaini yangu kuwa miradi hii iliyotiliwa saini leo itaenda kutekelezwa kwa wakati uliyopangwa ili wananchi waweze kufurahia huduma na miradi hii mbali na uboreshaji wa miundombinu hii lakini inaenda kuleta ajira kwa wananchi”amesema Sawala

Mratibu Msaidizi Mradi wa TACTIC kutoka Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Emmanuel Manyanga amesema utekelezaji wa mradi huo utahusisha ujenzi wa barabara za chuno kilometa 3.38,  barabara ya Samia City Access kilometa 2.4.

Pia mitaro ya kiyangu kilometa 1.73, kituo cha wajasiliamali eneo la Skoya, Stendi Kuu ya Chipuputa pamoja na jengo la una uratibu wa miradi usimamizi ambapo  mkataba wake ni wa miezi 15 kuanzia Oktoba 15, 2025 hadi Januari 14, 2027 chini ya mkandarasi M/S Serengeti Limited.

“Faida ya miradi hii ni kubwa ikiwemo uboreshaji wa hali ya biashara kwenye maeneo husika, kuwaondolea changamoto za mafuriko na mengine”amesema Manyanga

Baadhi ya wananchi waliyohudhuria ghafla hiyo ikiwemo Saidi Chande ameishukuru serikali kwa kuwaletea miradi hiyo mikubwa ya kimkakati ambayo inaenda kuwaondolea changamoto ya mafuriko kwenye maeneo yao.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button