Sh Mil.85 kuboresha miundombinu mradi wa maji Makonde

SERIKALI imetenga kiasi cha Sh milioni 84.8 kuboresha miundombinu ya mradi wa maji wa Makonde uliopo Wilaya ya Newala mkoani Mtwara.

Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), mkoani Mtwara Mhandisi Primy Damas, amesema huo ni moja ya miradi ya kimkakati ambayo inatekelezwa na serikali mkoani humu.

Damas amesema hayo akizungumzia mikakati ya mkoa kufikisha huduma ya maji vijijini kwa asilimia 85 ifikapo 2025.

Advertisement

Amesema utekelezaji wa uboreshaji wa mradi huo utanufaisha wananchi 539,000 katika Wilaya za Newala, Tandahimba na Nanyamba mji Mkoani Mtwara.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Primy Damas

“Mradi wa Makonde ulikuwa na uchakavu wa miundombinu na sasa serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuuboresha na kuongeza huduma ya maji kwenye maeneo ya vijiji vya pembezoni,” amesema.

Damas ametaja mradi mwingine wa kimkakati kuwa ni mradi wa kutoa maji Mto Ruvuma kwenda Mji wa Mangaka Wilaya ya Nanyumbu, ambao utahudumia wananchi 81, 330 Nanyumbu.

Kwa sasa upatikanaji wa maji katika vijiji mkoani Mtwara umefikia asilimia 67.

Amesema utekelezaji wa miradi hiyo miwili itaongeza kasi ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini na kufikia asilimia 85 ifikapo 2025.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *