Shabiby: Bandarini kuna upigaji
Ataka watanzania kutoogopa uwekezaji
SAA chache baada ya tangazo la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera la kutoa kitita cha sh milioni tano kwa atakayefanikisha kupatikana kwa mwanafunzi Ester Mwanyilu wa kidato cha tano shule ya Sekondari Panda Hili, mwanafunzi huyo amepatika maeneo ya Mbalizi.
Sauti inayoelezwa kuwa ni ya mama mzazi wa mtoto huyo anasema kuwa Esther amepatika Mbalizi ambako alikuwa akiishi kwa mama mmoja ambaye ni fundi cherehani.
‘Alivyotoroka shule alikwenda kwa huyo mama na alibadilisha mavazi akawa anavaa Hijabu zile za kininja za kufunika uso na kubakiza macho tu na jina alibadilisha akawa aitwi tena Esthet anaitwa Erica.
”Amesema na kuongeza
“Baada ya taarifa kusambaa na picha yake, kuna mtoto wa mama yake mkubwa (Esther), alikuwa anaongea na binti mmoja kuhusu kupotea kwa Esther, huyo binti akasema mbona huyo binti unayemsema kuna mahali nimemuona yuko kwa mama mmoja Mbalizi lakini aitwi Esther anaitwa Erica.
“Alipoangalia picha akasema ni yeye kabisa..
ni yeye..pamoja na kwamba anajifunika tunashindwa kumtambua lakini ni yeye.
“Sasa yule binti mtoto wa mama yake mkubwa akaenda kumueleza mama yake mzazi, mama ake akaenda Polisi kutoa taarifa leo asubuhi Polisi wameenda kuzingira hiyo nyumba na walimkuta kweli Esther wakamkamata na uyo mama akakamatwa kwa ufupi taarifa nilizopata ndio hizo kutoka kwa babu yake na Esther mzaa mama.”Amesema mama uyo.
Mwanafunzi huyo alipotea tangu Mei 18, 2023 na jana Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili mtoto uyo aweze kupatikana.