Shaka: CCM tunajivunia mafanikio lukuki Zanzibar

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinajivunia mabadiliko makubwa yaliyofikiwa Zanzibar katika kipindi cha miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ambayo yamewafanya wananchi kujiamini na kujiitegemea kimaendeleo.
Hayo yamesemwa leo Januari 12, 2022 na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa,  Shaka Hamdu Shaka katika mahojiano maalum.
Amesema, Zanzibar imepiga hatua kubwa sana na Chama Cha Mapinduzi kinatoa pongezi za dhati kwa kazi kubwa iliyokwishafanywa na inayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya nane chini ya Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi it kiendelea  kuunga mkono juhudi za kukomesha ukandamizaji wa haki , ubaguzi, dhulma na manyanyaso.
 Katika kipindi cha miaka 59 ya Mapinduzi matukufu licha ya kuleta ukombozi kamili lakini  pia yamewafanya  wananachi kuwa na fikra huru  na kujitawala.”Amesema Shaka na kuongeza
“Kabla ya mapinduzi lipo tabaka lilokandamiza, kubagua na kuwapuuza wengine huku wananachi wakikosa haki za msingi na kutotumia fursa za kiuchumi sawa na utu wao  kutothaminiwa, na kupuuzwa.”
Amesema Mapinduzi ya mwaka 1964 ni ushahidi kuwa Zanzibar ilikuwa na watu waliokoseshwa elimu bora, kutomiliki uchumi, ardhi, kukosa makaazi bora na kunyimwa huduma za jamii.
Aidha, amesema Serikali zote ya Mapinduzi Zanzibat (SMZ) na Serikali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) zimetimiza wajibu wa kusimamia maendeleo.
“Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais Dk. Mwinyi baada ya miaka 59 wametafsiri mapinduzi ya ukombozi kuwa Mapinduzi ya kiuchumi. Maendeleo  yanayoonekana  sasa hayakuwepo miaka 200 ya utawala wa kikoloni. ” Amesema na kuongeza
” Kazi kubwa iliyofanywa na Chama cha ASP ilikuwa kuhakikisha utawala wa ukandamizaji, uonevu na ubaguzi wa huduma za jamii unakomeshwa katika visiwa vya Unguja na Pemba kwa sera ya mapinduzi ya ukombozi na kazi iliyobaki ni kujenga uchumi na maendeleo.
Amesema ni vyema kwa watendaji  waliopewa dhamana katika Serikali na taasisi za umma kuhakikisha  wanatimiza wajibu wao kwa kumsaidia Rais Dk. Mwinyi ili akamilikshe kazi ya kutekeleza mapinduzi ya kiuchumi na kuongeza Kasi ya kuleta maendeleo.
“Kazi ya kumwondoa mkoloni aliyetawala kwa ubaguzi na ukandamizaji imemalizika. Kazi iliyobaki ni kuongoza kwa haki, umoja na maendeleo. Kukumbuka madhila yaliyokuwepo kabla ya mapinduzi kunatupa ari ya kufikia mabadiliko tuanayoyataka.”Amesema
Amesema, baada  ya kufanikisha mapinduzi ya mwaka 1964 na utawala kushikwa na ASP, Rais wa kwanza wa Zanzibar hayati Mzee Abeid Amani Karume alianza utekelezaji  wa sera za maendeleo ikiwemo kutolewa bure kwa huduma za msingi.
“Elimu imetolewa bure, maji  safi na matibabu, serikali ikaweka viwango vya mishahara minono kwa mujibu wa ajira ya kila mfanyakazi, yamejengwa makaazi ya kisasa na sasa kazi hiyo inaendelezwa na  serikali ya Rais Dk. Mwinyi.” Amesema Shaka
Amewataka watanzania hasa vijana kutobabaishwa na porojo za baadhi ya wapinga maendeleo na mapinduzi matukufu ya 1964 ambao wamekuwa wapotoshaji wa ukweli kwa kudai serikali ya  CCM haijafanya lolote tangu mwaka 1964 wakati asiliamia 98 ya maendeleo yaliyofanyika nchini yamepatikana katika utawala wa Chama Cha Mapinduzi.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x