Shambulio la M23 laua wanajeshi wawili wa Tanzania

Vikundi vya Tanzania vilivyopo DRC vipo salama, imara na vinaendelea kutekeleza majukumu yake

DODOMA – Tanzania imesema askari wake wawili wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) waliokuwa wakishiriki shughuli za ulinzi wa amani wameuawa kufuatia shambulio la Waasi wa M23 huko Goma, nchini DRC.

JWTZ imesema kupitia taarifa kwa vyombo vya habari kuwa katika shambulio hilo wanajeshi wengine wanne wamejeruhiwa.

“Taratibu za kuisafirisha miili ya marehemu pamoja na majeruhi zinaendelea kupitia Sekretarieti ya SADC,” Kanali Gaudentius Ilonda, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania amesema. 

Advertisement

Ameeleza kuwa wanajeshi hao walikuwa sehemu ya kikosi cha ulinzi wa ama cha Umoja wa Mataifa na Jumuiya za Kikanda.

Kwa mujibu wa Kanali Ilonda, vikundi vya Tanzania vilivyopo DRC vipo salama, imara na vinaendelea kutekeleza majukumu yake kwa maelekezo ya uongozi wa SADC .

JWTZ limeshiriki kulinda amani katika nchi mbalimbali ikiwemo Lebabon, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Liberia, Msumbiji, na DRC.

 

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *