Shamsa Ford: Punguzeni kuniomba fedha

MWIGIZAJI Shamsa Ford amesema  watu wamekuwa wakimpigia simu na kumtumia ujumbe kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii kumwomba fedha.

Akizungumza Dar es Salaam jana nyota huyo alisema kuna mtu aliomba amsaidie Sh milioni 22 akamalizie nyumba yake, akisema yeye hana fedha kwani anapambana na mikopo ili maisha yake yaende.

“Hii ni mara ya sita kupigiwa simu na meseji nyingi kuniomba pesa. Huyu wa leo (jana) alisema anaomba nimsaidie Sh milioni 22 akamalizie nyumba yake, mimi mbona sina mbwembwe zozote zinazoonesha nina pesa,” alisema na kuongeza:

“Jamani kuonekana kwenye televisheni haimaanishi nina pesa nyingi. Mimi mwenyewe napambana na mikopo, michezo ya vikoba ili maisha yaende, ndugu zangu punguzeni kuniomba pesa sina kitu,” alisema hayo Dar es Salaam jana.

Shamsa amekuwa akiigiza kwenye tamthiliya mbalimbali za televisheni na pia ni mjasiriamali wa nguo. Amekuwa akifanya shughuli hizo kuendesha maisha yake kwa muda mrefu.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button