Shekhe mkuu Mwanza ahamasisha siasa safi

SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (BAKWATA), Hassan Kabekhe amewataka viongozi na raia mbalimbali kuachana na siasa za matusi na uchochezi bali wafanye siasa nzuri.
Kabekhe ametoa wakati wa kongamano la wadau wa dini liliofanyika leo Oktoba 11 jijini Mwanza.
Amesema matusi na uchochezi hayatakiwi kabisa kwakuwa sio maadili ya Tanzania.
Katika hatua nyingine, Kabekhe amesema kutakuwa na mfungo malumu kwa waislam kwajili ya kuombea uchaguzi mkuu na amani, ambapo mfungo huo utaanza Oktoba 23- Oktoba 30. Amewaomba waislam kufunga na kuiombea nchi.
Naye Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA), Zainabu Haruna amewaomba wanawake wa dini ya kiislamu na wanawake wengine wote nchini kujitokeza kwa wingi siku ya Uchaguzi mkuu Oktoba 29 na kupiga kura.
Amewaomba wanawake wa dini ya kiislamu na wanawake wengine wote nchini kujitokeza kwa wingi siku ya Uchaguzi mkuu Oktoba 29 na kupiga kura.
Haruna amesema ni wakati sasa wanawake kujitokeza kwa wingi na kupiga kura ikiwa ni takwa la msingi la katiba. Amesema kupiga kura ni jukumu kubwa sana hivyo ni vyema kujitokeza na kupiga kura.
Kwa upande wake, Shekh wa Wilaya ya Ilemela, Abdulwarithi Juma amewaomba watanzania wote kwa ujumla kuhakikisha wanapiga kura kwa wakati kisha wanarudi nyumbani na kupumzika huku wakisubiria Tume iweze kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa ngazi mbalimbali.
Amewaomba Watanzania kutojaribu wala kufikiria kujihusisha na maandamano wala vurugu zozote katika siku ya uchaguzi.
Aliyekuwa Waziri wa utalii ,Lazaro Nyalandu amepongeza viongozi wa dini kwa mchango wao katika kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu. Amewaomba watanzania kupiga kura siku ya Uchaguzi.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com