Shirika latoa msaada huduma za afya

Shirika la “Madaktari Afrika” lililopo nchini Marekani limetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh bilioni 1 ambavyo vitatumika katika kambi maalumu ya siku tano ya matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo.

Kambi hiyo iliyoanza leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imelenga kubadilishana uzoefu baina ya wataalam wa afya wa JKCI na wenzao kutoka katika shirika hilo.

Akizungumza na madaktari wanaotoa matibabu katika kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel amewashukuru madaktari hao kwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na wataalam wa JKCI kuokoa maisha ya watanzania na kusemaa magonjwa ya mfumo wa umeme wa moyo ni sehemu ngumu kwenye masuala ya tiba ya moyo.

“Rais wetu alishawekeza mtambo wa kisasa wa kutibu umeme wa moyo, upande wa suala la tiba tumejitahidi kupata wataalam wenye uwezo wa kutoa huduma bora kuendana na teknolojia iliyopo, hatuna budi kushirikiana nanyi kwani muda mrefu mmekuwa mkitoa matibabu haya”, alisema naibu waziri.

Aidha alisema, mbali na kubadilishana uzoefu madaktari hao wamekuja wakijua yakuwa kuna watanzania wenye matatizo ya umeme wa moyo lakini hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu na hivyo kuleta vifaa vya matibabu kuwatibu wasiokuwa na uwezo wa kugharamia matibabu.

Habari Zifananazo

Back to top button