Shule za msingi, sekondari zapatiwa mipira Mwanza

SHULE 145 za msingi na 60 za Sekondari kutoka Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza zimepatiwa mipira ya miguu zaidi ya 400 kutoka taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Sports Charity.

Akizungumza katika hafla fupi ya ugawaji wa mipira hiyo iliyofanyika leo katika uwanja wa Mirongo, Mwenyekiti wa sports Charity, Rogasian Kaijage amesema mipira hiyo wametoa kwa lengo la kuinua michezo mashuleni.

Kaijage amesema zoezi hilo ni endlevu na wataendlea kutoa mipira ya miguu, mipira ya pete na mipira ya mikono kwa shule zote za halamshauri ya mkoa wa Mwanza.

‘’Zoezi hili ni endelevu na tutaendlea kugawa mipira kwa shule zote za mkoa wa Mwanza. Pia tutagawa mipira kwa vituo mbali mbali vya michezo kutoka maeneo tofauti’’ amesema Kaijage.

Naibu Meya wa jiji la Mwanza Bhiku Kotecha amesema anaishukuru sana taasisi ya Sports Charity kwa msaada huo wa mipira.

Amewaomba walimu wa michezo wa shule zote za mkoani Mwanza kuhakikisha wanaitunza mipira hiyo.

Mwalimu wa michezo wa shule ya Nyakabungo Haidari Abdul amesema mipira waliopewa itawasaidia sana katika kuinua vipaji vya mpira wa kikapu katika shule yao

Habari Zifananazo

Back to top button