Siku 100 za Rais Samia zinavyoashiria mapinduzi ya kilimo

KATIKA siku 100 za mwanzo za uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea na Halmashauri jirani ya Madaba wameanza kushuhudia kile kinachoweza kuitwa mwanzo wa mapinduzi ya kilimo Mkoani Ruvuma.
Serikali imepeleka jumla ya matrekta 15 katika mkoa huo, matano yakielekezwa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, matano Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru na matano Halmashauri ya Wilaya ya Songea, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuifanya sekta ya kilimo kuwa injini halisi ya uchumi mkoani humo.
Mhimili wa uchumi wa Ruvuma
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa maeneo nchini ambako zaidi ya asilimia 75 ya wananchi hutegemea kilimo kama chanzo kikuu cha kipato. Mazao kama mahindi, kahawa, korosho na maharage yamekuwa uti wa mgongo wa uchumi wa kaya nyingi.
Hata hivyo, changamoto za muda mrefu, ikiwemo matumizi ya zana duni, gharama kubwa za uzalishaji na kuchelewa kwa maandalizi ya mashamba, zilikuwa zikidhoofisha juhudi za wakulima kuimarika kiuchumi. Kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali ya Awamu ya Sita imeanzisha mpango wa kusambaza zana za kisasa ili kuongeza uzalishaji, kupunguza gharama na kuwavutia vijana kuona sekta ya kilimo kama ajira yenye tija.
Akizungumza wakati wa kupokea matrekta hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Elizabeth Gumbo anasema ujio wa zana hizo ni hatua muhimu katika safari ya kuikomboa sekta ya kilimo katika halmashauri hiyo.
“Halmashauri yetu inategemea sana kilimo. Matrekta haya yatawaweze sha wakulima kulima kwa wakati, kuongeza ukubwa wa mashamba na hatimaye kuongeza kipato cha familia nyingi. Hii ni chachu ya maendeleo ya kweli,” anasema.
Takwimu zinazobashiri mabadiliko
Uwekezaji katika kilimo hauishii kwenye matrekta pekee. Kwa mujibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kupitia Idara ya Uchumi na Uzalishaji, maofisa ugani 370 wanahudumia wakulima katika ngazi ya kata na vijiji huku pikipiki 242 na vishikwambi 213 vikitumika kuboresha utoaji wa huduma mashambani.
Ekari 10,632 zimepimwa afya ya udongo mkoani Ruvuma na wakulima 31,295 wamepatiwa elimu ya udongo. Zaidi ya wakulima 287,051 wamesajiliwa kwenye mfumo wa ruzuku ya pembejeo kupitia vituo 202 na mbolea aina mbalimbali zimesambazwa kwa wakulima, hatua inayoongeza tija na uzalishaji.
Matumizi ya zana za kisasa yameongeza kasi ya maandalizi ya mashamba, kupunguza uchovu wa wakulima na kuongeza mavuno ni dalili zinazoashiria mageuzi yanayochukua sura mpya vijijini. Sauti kutoka mashambani kwa wakulima wanaona matrekta hayo si vifaa tu, bali alama ya matumaini mapya katika safari yao ya kiuchumi kupitia sekta hiyo.
Mkulima wa Kijiji cha Mpitimbi, Joseph Ngongi anasema “Zamani tulikuwa tunachoka sana kulima kwa jembe la mkono. Wakati mwingine mvua zilianza kabla hatujamaliza kuandaa shamba. Sasa trekta linamaliza kazi kwa siku chache. Changamoto iliyobaki ni kuhakikisha matrekta yanapatikana kwa wakulima wote kwa wakati na gharama nafuu,” anasema.
Kwa upande wake, Sophia Komba anaona mabadiliko haya kama mlango wa kuingia kwenye kilimo cha biashara. “Gharama zimepungua na eneo ninalolima limeongezeka. Sasa nafikiria kuuza zaidi sokoni badala ya kulima kwa ajili ya familia tu. Pendekezo langu ni serikali iendelee kuongeza zana hizi ili vijana wavutiwe kuja mashambani,”anaeleza.
Si wakulima wanawake ndio wanaonufaika; mkulima wa mahindi wa Kijiji cha Lipaya, John Ngatunga anasema ujio wa matrekta hayo umeondoa hofu ya kupoteza msimu. “Changamoto yetu ilikuwa kuchelewa kulima, na hilo lilipunguza mavuno. Hali sasa ni bora, tunapanda kwa wakati. Tunashauri kuwe na ratiba wazi ya matumizi ya matrekta ili kuepuka msongamano wakati wa msimu,” anasisitiza.
Kwa upande wake Jenista Ndunguru, mkulima na mama wa watoto wanne anasema, “Kilimo kinapokuwa rahisi, hata maisha ya familia yanabadilika. Tunaweza kugharamia elimu ya watoto. Hata hivyo, tunahitaji mafunzo zaidi ya matumizi bora ya pembejeo ili mavuno yaendane na uwekezaji wa zana.”
Upatikanaji wa matrekta Kwa mujibu wa Mratibu wa zana za kilimo wilayani Songea, Mathias Ambros, mkulima anayehitaji huduma ya trekta anatakiwa kuwasiliana na Ofisa Kilimo wa kata au mratibu ili apangiwe ratiba. Utaratibu huo unalenga kuhakikisha uwazi, usawa na ufanisi katika matumizi ya rasilimali hizo muhimu.
Hatua hii inaendana na Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2013 inayosisitiza matumizi ya teknolojia za kisasa kuongeza tija na ushindani wa mazao ya Tanzania ndani na nje ya nchi.
Pia, utekelezaji wake unahusiana na mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, unaotambua kilimo kama kichocheo cha ukuaji wa uchumi sambamba na Sheria ya Sekta ya Kilimo na Ushirika, inayohamasisha uwekezaji na ushiriki wa sekta binafsi, pamoja na Ajenda ya Kimataifa ya Kilimo Himilivu Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi, inayosisitiza matumizi ya zana rafiki kwa mazingira.
Katika hatua inayothibitisha dhamira ya serikali, Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ametangaza mpango wa kununua matrekta 10,000 na kuanzisha vituo jumuishi 1,000 vya zana za kilimo katika ngazi ya kata.
Mpango huo unalenga kuongeza tija mashambani, kupunguza gharama za uzalishaji, kutoa muda kwa wakulima kushiriki shughuli nyingine za kiuchumi na kuwashirikisha vijana na wanawake katika biashara ya zana za kilimo Elimu na teknolojia Maofisa ugani wameendelea kutoa mafunzo kupitia mashamba darasa kuhusu afya ya udongo, matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu, kilimo hifadhi, umwagiliaji na masoko na gharama za uzalishaji.
Taswira mpya vijijini
Mabadiliko haya yanaanza kuonekana wazi kwa wakulima kuongeza ukubwa wa mashamba, maandalizi ya haraka na wakulima wanaozungumza kwa kujiamini kuhusu masoko badala ya kuishia kwenye uzalishaji wa kujikimu pekee.
Kwa wengi, hii ni tafsiri halisi ya falsafa ya Serikali ya Awamu ya Sita, kuwafikia wananchi moja kwa moja na kubadilisha maisha yao kupitia miradi yenye matokeo yanayoonekana. Simulizi ya matrekta Ruvuma si tu kuhusu mashine zinazoingia mashambani, ni simulizi ya matumaini yanayochipua, jasho la mkulima linalopata thamani na uchumi wa vijijini unaoanza kusimama kwa uimara.
Ingawa bado kuna haja ya kuongeza rasilimali; kuimarisha ratiba za matumizi na kuendelea kutoa elimu kwa wakulima, ishara zilizopo zinaonesha wazi kuwa Tanzania inaelekea kwenye kilimo cha kisasa chenye tija.




Hatimaye Samia Amuua Angani Kwa Bastora
https://youtu.be/0Bs8W3BfiWE?si=KJVHFDrS-fv6hx5p
I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com
Hatimaye Samia Amuua Angani Kwa Bastora
.
https://youtu.be/0Bs8W3BfiWE?si=KJVHFDrS-fv6hx5p