Simba haitaki unyonge

DAR ES SALAAM: NAHODHA wa Simba ya Dar es Salaam, John Bocco amesema kikosi chao kimejiandaa vizuri kukabiliana na Al Ahly ya Misri mchezo wa ufunguzi michuano mipya ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) kesho Oktoba 20, 2023 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
–
Pia amesema kurejea kikosini kwa beki Henock Inonga kumezidi kuimarisha timu yao kwa ajili ya mchezo huo.
–
“Utakuwa ni mchezo mkubwa kwa Afrika yetu na Tanzania kwa ujumla, tunategemea kuonesha mchezo mzuri na wa kiungwana kwa wapinzani wetu,” amesema Bocco
–
“Mchezo utakuwa mgumu lakini mwalimu ametuandaa vizuri na tunaomba mashabiki washirikiane nasi. Tunatarajia matokeo mazuri kwani tuna wachezaji wazuri wenye ubora na uzoefu kucheza michezo ya aina hii katika kikosi chetu,” amesema nahodha huyo.
–
“Tuna wachezaji wazuri na tumefurahi kurejea kikosini kwa mwenzetu, Henock Inonga baada ya kuwa majeruhi kwa majumaa kadhaa, na bila shaka yupo tayari kwa mchezo wa kesho, kinachobaki ni mipango tu ya mwalimu na benchi lake la ufundi,” amesema Bocco.
My last pay check was $9500 working 12 hours a week online. My sisters friend has been averaging 15k for months now and she works about 20 hours a week. I can’t believe how easy it was once I tried it out.
This is what I do…. http://Www.Smartcash1.com