DAR ES SALAAM;Haiishi mpaka iishe! Pengine ndivyo unwvyoweza kuzungumzia matokeo ya mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) kati ya Simba na CS Sfaxien uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao2-1.
Bao la dakika ya 90+7 lililofungwa na Kibu Dennis liliihakikishia Simba ushindi na kuibua furaha kwa mashabiki timu hiyo, wakati wakiamini matokeo yangekuwa sare ya 1-1.CS Sfaxien walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya tatu, kisha Kibu kuisawazishia Simba dakika ya 7.