WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuchukua hatua kwa kuwaandikia timu ya Simba SC na kuwanakiri Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF) ili gharama za uharibifu wa viti uliosababishwa jana zilipwe.
Wakati huo huo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imelaani vitendo vya mashabiki kung’oa na kuharibu viti katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, kati ya Simba SC ya Tanzania na Club Sportif Sfaxien ya Tunisia uliofanyika jana.
Mheshimiwa Waziri Kabudi amewataka mashabiki wanaoingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuacha vitendo vya uharibifu wa uwanja, kwa kuwa wanasababisha hasara kwa Serikali na kuharibu ubora wa uwanja.