Simba mawindoni Ligi Kuu leo

Kikosi cha Simba kilichoanza katika moja ya michezo ya timu hiyo.

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kufanyika Dar es Salaam.

Klabu ya Simba itakuwa wenyeji wa KMC kwenye uwanja wa KMC Complex, Mwenge Manispaa ya Kinondoni.

Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 22 baada ya michezo tisa wakati KMC ni ya saba ikiwa na pointi 14 baada ya michezo 10.

Advertisement

SOMA: Viwanja 3 kuwaka moto Ligi Kuu leo

Katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa Novemba 5, Pamba Jiji imeona mwezi baada ya kushinda mechi ya kwanza Ligi Kuu dhidi ya Fountain Gate kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa kwa mabao 3-1.