SIMBA itakuwa ugenini leo kuikabili Pamba Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tan zania Bara, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Wekundu hao wa Msimbazi wa naongoza ligi wakiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 10, mchezo uliopita walishinda mabao 4-0 dhidi ya KMC katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. na aliwapa mazoezi mepesi kabla ya mchezo wa leo.
Akizungumza kuelekea mchezo wa leo, Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids alisema anatarajia up inzani mkubwa lakini malengo yake ni kupata pointi tatu akiwa ugenini.
Pamba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fred Felix ‘Minziro’ wanai karibisha Simba wakiwa na rekodi ya kupata ushindi wao wa kwanza chini ya nahodha huyo wa zamani wa Yanga baada ya kuifunga Foun tain Gate mabao 3-1, Uwanja wa Tanzanite, Babati mkoani Manyara.
Kwa sasa wanashika nafasi ya 15 wakiwa na pointi nane baada ya ku cheza mechi 11, wakishinda mchezo mmoja, wametoka sare mara tano na kufungwa michezo mitano.
“Nimeutumia vizuri muda wa mapumziko kukiandaa kikosi nilichobakinacho baada ya wengine kuwa na timu zao za taifa na tuko tayari kupata pointi tatu dhidi ya Pamba,” alisema Fadlu.
Alisema wachezaji waliokuwa na timu zao za taifa wote wamerejea Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Pamba, Minziro alisema anatarajia mchezo mzuri wenye ushindani kwa sababu kikosi chake kimeimarika.
“Unajua timu inapokuwa haishindi inakuwa na presha, lakini baada ya kupata matokeo hali imebadilika, kesho (leo) tutegemee mchezo mzuri na si kitu kingine zaidi,” alisema Minziro