Simba SC mwaka wa tabu

Simba SC imeendelea kuangusha pointi kwa mara nyingine baada ya leo kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo, mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Namungo ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 29 lililofungwa na Reliants Lusajo dakika ya29.

Jean Baleke alifunga bao la kusawazisha dakika ya 75 na mchezo kuisha hivyo.

Advertisement

Matokeo hayo yanaiweka Simba SC nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi, ikiwa na pointi 19, wakati Yanga ikiongoza kwa pointi 24.

1 comments

Comments are closed.