KLABU ya Simba imetangaza kuachana na mlinda lango wake Beno Kakolanya mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake.
Kwenye taarifa iliyotolewa Juni 22,2023 kwenye kurasa za mitandao za Simba timu hiyo imemshukuru Kakolanya kwa mchango wake kwenye kikosi hicho cha mitaa ya Msimbazi Dar es Salaam.
“Uongozi wa klabu unaujulisha umma kuwa hatutaendelea kuwa na mlinda mlango, Beno Kakolanya baada ya mkataba wake kumalizika,” imesema taarifa hiyo.
Comments are closed.