“NILISIKIA kama tetemeko ambalo huwezi kujua limetokea wapi na ile kuangalia juu, nikaona nyufa na ukuta unatikisika.
“Nilipotaka kutoka, nikaona kitu kama kinanivuta, nikaanguka palepale kwenye mezani kwa chini.” Mmoja wa majeruhi katika ajali ya kuporomoka kwa jengo katika Kata ya Kariakoo Dar es Salaam, Novemba 16, 2024 Benedicto Raphael anasema akisimulia namna yeye na wenzake walivyokumbwa na masaibu ya kuporomoka kwa jingo hilo na kusababisha wengine kupoteza maisha huku yeye akiwa chini ya kifusi hadi alipookolewa baada ya siku tatu.
Akizungumza na wananchi na waokoaji waliokuwa Karia koo juzi baada ya kutoka nchini Brazil alikohudhuria Mkutano wa G20, Rais Samia Suluhu Hassan alisema waliothibitika kufariki dunia kutokana na mkasa huo ni watu 20 waki wamo wafanyabiashara, wafan yakazi, wageni na wanunuzi wa bidhaa.
Baada ya kuzungumza katika eneo la tukio, Rais Samia alizuru majeruhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI).
Soma pia:Tume kuchunguza ubora wa maghorofa Kariakoo
Akisimulia mateso aliy opata akiwa chini ya kifusi na wenzake, Benedito anasema kutokana na hali waliyokuwa nayo chini ya kifusi, kadri muda ulivyozidi kwenda, ndivyo naye alivyozidi kupo teza tumaini la kuokoka au kupatikana ama akiwa hai au amekufa. Benedicto alikuwa akifanya biashara katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.
Anasema akiwa katika ulimwengu huo wa mashaka, hakuwa anafahamu muda wala likichokuwa kinaendelea.
“Kule nilikuwa sihesabu siku maana sijui ni mchana au ni usiku na wala sijui ni saa ngapi… Mimi ni kulala na jigeuza upande huu nikichoka nageuka upande huu nikisubiri maombi ya watu,” anasema.
Anaongeza, “Huwezi jua kama ni mchana au ni usiku, ni giza nilisikia Jeshi la Zimamoto wakiniita wananiuliza unaona mwanga nikawaambia hapo sioni wanakuja upande wa pili wananiuliza unauona mwanga nikasema, naona.”
Kwa mujibu wa manusura huyo, alilazimika kutafuta walipo waokoaji kwa kuso gea taratibu akifuata sauti na mwanga na kupata msaada. Anasema kilichomsaidia kutoka katika kifusi kile ni mawasiliano baina yake na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
“Tulikuwa tunawasiliana, Tulikuwa tumemaliza shughuli zetu tumekaa ghafla tukashangaa tumepata kama vile tetemeko tutakosa jinsi ya kutoka tukaporomokewa… Ilikuwa kama saa mbili hivi asubuhi,” anasema na kuongeza, unatuona anasema nawaona sogea upande wa pili nasogea, na mwisho nikatoka,” anasema akishukuru jeshi hilo na jitihada za Serikali na Watanzania wote kwa ujumla kwa maombi na msaada uliookoa maisha yake.
Wakati Benedicto akiwa amekaa kwa siku tatu chini ya kifusi, Yasinta ambaye pia ni manusura katika ajali hiyo yeye anasema alikaa chini ya kifusi kwa masaa 12 na baadae aliokolewa pamoja na wenzake.
“Tangu saa tatu asubuhi tumetoka saa tatu asubuhi Jumapili, saa 12 nilikuwa nime fukiwa kabisa na kifusi mpaka sasa hivi mguu haufanyi kazi, nimetoka nikiwa hai namshu kuru Mungu,” anasema Yasinta na kubainisha kuwa, mmoja wa watu aliokuwa nao aliwapigia simu ndugu zake na ndipo wakapata msaada kutoka kwa wanajeshi.
Anasisitiza, “Michael alikuwa na simu akatusaidia, akawapigia ndugu zake ndio wanajeshi wakatufikia. Kwa jinsi nilivyookolewa, serikali inafanya kazi tulisali sana na tuliita sana wanajeshi wakaja kutusaidia tunashukuru sana.”
Katika matukio kama haya taarifa za upotoshaji pia zimekuwa haziko mbali kwani wapo waliozushiwa kuwa wamefariki, jambo ambalo lilisononesha jamii kwa kiasi kikubwa na kuzua taharuki katika familia kuwa wamefiwa ndugu yao kumbe si kweli. Hassan Mwampamba anasimulia kilichotokea baada ya jengo kuporomoka.
Anasema, “Wakati jengo linaanguka tulikuwa 26, kwanza tulichagua viongozi wa kudhibiti ile hali kwa sababu watu walikuwa wanalia sana, mule ndani kulikuwa na maji; tukagawana wote.
Tulitafuta sehemu yenye mwanga tuka omba msaada…” Mwampamba anasema kutokana na sehemu ulipopita mwanga katika kifusi hicho kuwa ndogo, walitumia fimbo kuomba msaada.
“Tukaonesha kifimbo kuombea msaada kwa sababu mkono ulikua haupiti baadae tulipopata nafasi ya kupita tukaitumia kuwatoa wen zetu kisha na sisi tukafuata,” anasema.
Anasema hata yeye alipata mshituko kwa kusambaa kwa taarifa kwamba amekufa. “Tulivyofika Muhimbili ndio nikaona taarifa kuwa mimi nimefariki nikaawambia mimi nipo hai mtandao tu ulikata na ile picha nilipiga kama ukumbusho,” anasema.
Naye Nobert Oswad anas ema alifikiswa hospitali akiwa hajitambui. Kuhusu hali ya maisha chini ya janga la kifusi, anasema, “Tulikuwa tunakosa pumzi tunakosa pa kutokea sijatege mea kama nitafika hapa.
“Nilikuwa na hali mbaya sielewi kama mwenzangu yupo au alishafariki.” Manusura hao wanasema changamoto kubwa walioy pita wakiwa chini ya kifusi, ni kukosa hewa.
Linda Kwai anasema chini ya kifusi walikuwa hawawezi kuona na wakati mwingine walikosa pumzi kabisa. “Tulikuwa tumemaliza shughuli zetu tumekaa ghafla tukashangaa tumepata kama vile tetemeko tutakosa jinsi ya kutoka tukaporomokewa… Ilikuwa kama saa mbili hivi asubuhi,” anasema na kuongeza,”
“Tulikuwa tunakosa pumzi na hatuoni tunapotokea kulikuwa na giza sana”. Anadokeza kupona kwao akisema, “Tulimpigia mkuu wa mkoa (Dar es Salaam, Albert Cha lamila) akawatuma wanajeshi (waokoaji) wakaja kutuokoa, bila wao tusingetoka wametusaidia sana.”
Manusura mwingine aliyeteka hisia za wengi ni Jackson Clement ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne aliyekuwa kwenye mitihani yake ya kuhitimu elimu ya sekondari na kwamba, alikuwa amebakiza mtihani mmoja aliopaswa kufanya jana.
Anasema alikuwa amenasa kwenye kifusi baada ya jengo kuporomoka. “Nilistuka jengo tayari lishanifunika; nikajaribu kukimbia, lakini nilikuwa nimenasa juu kwenye nondo kifusi kilikuwa kingi… Siku ya pili nilianza kupiga kelele watu walinisikia wakaanza kufukua,” Anasema na kuongeza, “Hali ilikua ngumu sana…tulipiga kelele sana walitoboa na kupitisha maji”