SMZ kushirikiana na wataalam wa kimataifa

ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi  amesema Serikali itaendelea  kuunga mkono juhudi za taasisi za kitaaluma za kimataifa zinazoonesha dhamira ya  kushirikiana na Zanzibar  kuijengea uwezo  wa kielimu katika nyanja mbalimbali.

Dk.Mwinyi ameyasema hayo Ikulu  Zanzibar wakati alipokutana na  Mkuu wa  Chuo kikuu  cha Imperial cha  Uingereza  Profesa Lam Wamsley na Ujumbe wake Ikulu ndogo  Mtaa wa Laibon Dar es Salaam.

Aidha  Dk.Mwinyi  ameeleza  kuwa  bado nchi inahitaji kupanua wigo wa kitaaluma  katika juhudi za kuleta Maendeleo kukuza Uchumi na kuongeza maarifa na Ujuzi  wa  watu  wake.

Ameyataja maeneo ya  biashara, afya, utafiti na teknolojia ya mawasiliano  kuwa   muhimu kwa nchi  na kuelezea kuunga mkono  nia ya Chuo Kikuu cha Imperial cha  Uingereza   ya kufungua milango  ya ushirikiano wa kitaaluma  na  kuanzisha programu tofauti  kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Suza.

Halikadhalika Dk.Mwinyi amesisitiza kuwa   Zanzibar imeendelea  kuweka mkazo zaidi katika kuviimarisha Vyuo Elimu ya juu    ili kuandaa Wataalamu katika sekta mbalimbali  na kwamba  bado inahitaji kuungwa mkono   kimataifa.  SOMA : Zanzibar kuweka mkazo zao la mwani

Ujumbe huo  umekuja nchini kuangalia maeneo  ya ushirikiano  na hatimae kuanzisha programu za mafunzo .

Habari Zifananazo

Back to top button