SMZ, TTCL kuimarisha mawasiliano Zanzibar

ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amelihakikishia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) itaendelea kushirikiana nalo kuimarisha huduma za mawasiliano visiwani Zanzibar.
Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Machi 23, 2026, alipokutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTCL, David Nchimbi, aliyefika Ikulu Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha, akifuatana na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, CPA Moremi Marwa, pamoja na viongozi wengine wa shirika hilo.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk Mwinyi alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarishwa kwa miundombinu ya mawasiliano, akieleza kuwa sekta hiyo ni mhimili muhimu katika kukuza uchumi wa kidijitali, kuimarisha huduma za kijamii kama elimu na afya mtandao, pamoja na kuchochea uwekezaji na utalii Zanzibar.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, David Nchimbi, alimshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa ushirikiano mzuri unaoendelea kati ya shirika hilo na SMZ, akibainisha kuwa TTCL itaendelea kutoa huduma bora na za kisasa ili kukidhi mahitaji ya wananchi na kuchochea maendeleo ya Tehama nchini.

Aidha, alieleza kuwa kuimarika kwa mawasiliano Zanzibar kutaleta manufaa makubwa kwa TTCL, ikiwemo kupanua wigo wa soko, kuongeza idadi ya wateja wa huduma za intaneti na mawasiliano ya simu, pamoja na kukuza mapato ya shirika.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com