WANANCHI mkoani Songwe wamepewa elimu ya namna ya kunufaika na taasisi ya imarisha uchumi na Mama Samia (IMASA) lengo likiwa ni kuhakikisha akina mama, wazee, vijana na watu wenye ulemavu wanainuka kiuchumi.
Katibu Mtendaji kutoka NEEC, Bengi Issa akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wilayani Mbozi amewaeleza mamia waliofika kwenye mafunzo hayo namna taasisi hiyo itakavyowanufaisha wananchi .
Bengi amesema program hiyo itahakikisha kuwapatia elimu ya namna ya kupata uwezeshwaji kutoka kwa Rais Samia kupitia taasisi ya IMASA.
SOMA: Bil 19/- zawezesha vikundi kujiinua kiuchumi
Amesema Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi ndio msimamizi mkuu wa program hiyo kwa kushirikiana na ofisi za wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi wa manisipaa, halmashauri za wilaya, Jiji na wadau katika maeneo husika.
“Madhumuni ya kutembelea mikoa yote 26 ya Tanzania Bara nikuhakikisha wanapata takwimu sahihi za wananchi waliopo kwenye maeneo husika na shughuli wanazozifanya za kiuchumi pamoja na kupata majukwaa ya uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi ambapo hadi sasa bado mikoa 5,”amesema.
SOMA: Watuhumiwa 11 wa uganga wanaswa Songwe
Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Ushiriki wa Watanzania kwenye Uwekezaji, Neema Mwakatobe amesema program hiyo itatekelezwa kwa awamu mbili ambapo amesema awamu ya kwanza ni uandaaji kanzi data ya walengwa na wanufaika wa programu ikiwa ni ni pamoja na utambuzi wa shughuli za kiuchumi za wadau na mahitaji maalumu ya uwezeshaji.
“Awamu ya pili italenga uandaaji wa program maalumu za uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake, Vijana, wazee na wanye ulemavu kuingana na mahitaji yayaliyoone kana katika uchakataji wa takwimu na kuanza utekelezaji.