Stephen Curry aumia kifundo cha mguu

NYOTA wa kikapu wa Golden State Warriors, Stephen Curry huenda akawa nje kwa michezo kadhaa baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Clippers jana.

Curry, 36, alitolewa katika mchezo huo katika robo ya tatu na kupokea matibabu huku taarifa zikieleza kuwa anasumbuliwa na enka.

MVP mara mbili alirejea mchezoni dakika nne baada ya robo ya nne lakini maumivu yalizidi na kuondolewa moja kwa moja na mchezaji mwenzake, Gary Payton hadi chumba cha kubadilishia nguo.

“Ni wazi ameteguka kifundo cha mguu imekuwa mara nyingi hapo. Sio  mbaya sana, lakini ni wasiwasi,”  Steve Kerr kocha wa Warriors alisema.

SOMA: Historia yaandikwa NBA