MWIGIZAJI wa vichekesho Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ amempa tano Rais Samia Suluhu Hassan na kutoa pongezi kwa Wizara ya Utalii na Maliasili chini ya uongozi wa Dk Pindi Chana kwa kuliingizia taifa Pato kubwa kupitia utalii.
Hayo ameyasema Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo baada ya kushiriki hafla ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
“Tuchukue nafasi hii kuipongeza wizara ya utalii kwa kuendelea kuwa wabunifu na kuendelea kuliingizia pato kubwa Taifa kupitia Utalii,
“Tunachukua nafasi hii kumkushuru Katibu Mkuu kuu Dk Hassan Abasi kwa kufungua njia na milango katika kuhakikisha utalii wa ndani unakua kwa kiasi kikubwa.
“Sisi kama mama ongea na mwanao tutashirikiana na wizara hii kukuza utalii wa ndani kuhakikisha tunautangaza, tunalinda na tunaudumisha,”alisema.