SUA yapata mashine mpya kuchakata mazao ya misitu

CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Morogoro (SUA), kimenunua mashine mpya ya kuchakata mazao ya misitu yenye thamani ya Sh milioni 200.

Mashine hiyo aina ya Slidetec Sawmill 2020  ina uwezo wa kuchakata mbao mita za ujazo 10 hadi 15 kwa saa 8, kwani awali kulikuwa na mashine na kuleta ufanisi zaidi kwa wanafunzi wanaosoma masomo hayo ya mazao.

Akizindua mashine hiyo sanjari na ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya Baraza la wajumbe wa chuo hicho leo katika kampasi ya Msitu wa Mafunzo wa Omotonyi jijini Arusha, Mkuu wa chuo hicho, Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Warioba amewataka wajumbe wa baraza la chuo hicho kuhakikisha tafiti za masuala ya misitu, kilimo na uvuvi zinaendana na mabadiliko ya tabianchi katika kutatua changamoto zinazohusiana na hali hiyo.

Amesema semina elekezi zinazotolewa kwa kila taasisi zina lengo la kuhakikisha ufanisi wenye tija ikiwemo weledi, uzalendo sanjari na matumizi sahihi ya fedha katika kuleta maendeleo chuoni hapo.

Makamu Mkuu wa chuo cha SUA, Profesa Raphael Chibunda amesema uwepo wa mashine hiyo ni uboreshaji wa mafunzo ya kisasa kwa vitendo na ina uwezo wa kuchakata mita za ujazo 10 hadi 15 kwa saa 8, kwani awali kulikuwa na mashine ya mbao inayochakata mbao mita za ujazo 5 hadi 7 kwa saa 11

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x