Washauri elimu adhabu mbadala

WANAJUMUIYA ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wameishauri Tume ya Haki Jinai kuweka mkazo wa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa adhabu mbadala badala ya kifungo, kwani waliowengi hawazifahamu na hawazipendi hizo adhabu mbadala zitumike .

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanajumiya wa chuo hicho katika wa mhadhara uliofanyika Agosti 24, 2023 na wajumbe wa tume hiyo wakiongozwa mjumbe wa tume ambaye ni  Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu,Balozi Ernest Mangu.

Mhandhiri mwandamizi wa chuo hicho, Profesa Yasinta Muzanila amesema hizo adhabu mbadala zikifahamika kwa jamii na kuona zinauzito wakutosha wataona pia zinafaa kusaidia kurekebisha tabia.

Akijibu maswali na maoni ya wanajumuiya hiyo  mjumbe wa tume hiyo ambaye Balozi Mangu amesema kuwa adhabu ni pamoja na kifungo cha nje .

Balozi Mangu amesema adhabu mbadala nyingine ni mfungwa kuwa chini ya usimamizi wa taasisi zilizopewa jukumu la kuangalia wafungwa.

Balozi Mangu aliwahakikishia kuwa maoni na ushauri uliotolewa wanajumuiya ya chuo hicho yamechukuliwa na yatawasilishwa wakati wa utekelezaji wa mapendekeo ambayo tayari wamewasilishwa kwa Rais.

Pamoja na hayo amesema tume hiyo kwa kushirikiana na vyombo vya habari inaendelea kutoa  elimu kwa wananchi kuhusu kutambua haki zao na wapi wanaweza kwenda kupata haki zao .

Januari 31 mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan aliizindua Tume ya Haki Jinai na alifikia uamuzi wa kuunda tume hiyo baada ya kusikia kwa muda mrefu kilio cha wananchi wakilalamikia juu ya huduma duni inayotolewa na taasisi zote za haki jinai  nchini.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button