Sudan Kusini yaiomba Marekani kurejea uamuzi wa kufuta viza

JUBA: SERIKALI ya Sudan Kusini imeiomba Marekani kuangalia upya uamuzi wake wa kufuta viza kwa raia wa Sudan Kusini ambao wametimiza masharti ya sheria za uhamiaji za Marekani.
Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Kusini inaonyesha kwamba nchi hiyo inajitahidi kuweka mazingira ya amani na usalama wakati ikisisitiza dhamira yake ya kusuluhisha suala hili kupitia mazungumzo yenye tija yanayozingatia viwango na sheria za kimataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ametangaza kwamba Uwanja wa Kimataifa wa Juba umekataa kuwapokea raia wa Sudan Kusini waliofukuzwa nchini Marekani.
Uamuzi huu wa Marekani wa kusitisha visa kwa Raia wa Sudan Kusini walioko nchini Marekani kuingia wasiwasi huku serikali yao ikiendelea na mazungumzo.



