Taarifa zisizo sahihi afya ya uzazi zinagharimu vijana

TAARIFA zisizosahihi kuhusu masuala ya uzazi imetajwa kugharimu maisha ya vijana wengi kutokana na imani mbalimbali ambazo zinazuka katika jamii.

Mkurugenzi wa Mtandao wa mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali Ukanda wa Afrika Mashariki (EANNOS) Onesmo Kalama amesema taarifa ambazo sio sahihi kuhusu afya ya uzazi zimekuwa zinagharimu maisha ya vijana wengi kutokana na kushindwa kutumia huduma zilizopo za uzazi ipasavyo.

“Kuna changamoto nyingi ambazo zinafanya vijana kushindwa kujiingiza katika afya ya uzazi moja wapo ni upatikanaji wa huduma haujakuwa rafiki sana kwa vijana kwa mfano ukianga sehemu nyingi ambazo vijana wanatakiwa kupata huduma wanaogopa kwenda kwasababu ni sehemu za watu mchanganyiko.

Ameongeza “Anaogopa akifika pale je akikutana na shangazi yake?atamwambia nimekuja kufanya nini katika klini ya akinamama akawa anaogopa na ikawa ni changamoto kwake kuja kupata huduma.

Amesema hali hiyo inawafanya wengi kukimbilia famasi kununua dawa bila kumuona daktari kwasababu dawa zingine anatakiwa kupata kutoka kwa daktari lakini wanajinunulia baada ya kupata taarifa kutoka kwa marafiki zao .
Kalama amesema hali hiyo inaleta athari kubwa katika miili yao hapo mbeleni lakini oia mila zinamuweka mtoto wa kike katika hali hatarishi mfano anapoolewa mapema kwa kulazimishwa huku bado wakiwa hawajakomaa.
“Vijana wa kiume hakujakuwa na mafunzo mambo mengi yanayozungumzwa yanakuwa ya kijana wa kike lakini wengi wa kiume wameachiliwa hawana muongozo,”alieleza Kalama.

Aidha amebainisha kuwa ni muhimu kupanua mazungumzo na uwepo wa utaratibu wa kuhakikisha vijana wanapata elimu sahihi kama sheria inavyosema kwa umri wao ili kwamba wasijiingeze kwenye mambo ambayo hayafai kuingia kwa umri wao.

“Kahiyo nafikiri kupeana elimu sahihi itakuwa vizuri na pia vijana kupewa huduma rafiki ili wanaweza kwenda vituo vya afya wakiwa na amani na kupata maelezo sahihi kulingana na afya yao ya uzazi.

Kwa upande wake mtengenezaji wa maudhui ya mtandao wa masuala ya afya ya uzazi kwa vijana, Lilian Lema alifafanua kuwa afya ya uzazi kwa vijana ni umuhimu sana kwababu inasaidia vijana kujikinga na magonjwa ya mfumo wa uzazi,hedhi salama na mimba zisizotarajiwa.

“Uzazi wa mpango zipo za aina nyingi kama dawa za kumeza,sindano,vijiti na kutumia kondom na faida yake ni kwamba zinamsaidia kijana kujikinga na mimba zisizotarajiwa na pia zinasaidia kijana au mzazi kupangilia idadi ya watoto,njia ya kondom inasaidia kuepukana na magonjwa ya ngono kwa watumiaji,”alifafanua Lema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Royal
1 month ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by. follow instructions on this website…….. http://Www.SmartCash1.com

KathleenCalvert
KathleenCalvert
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by KathleenCalvert
Julia
Julia
1 month ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18,000 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online.
.
.
Detail Here————————————————————>>>  http://Www.BizWork1.Com

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x