Taasisi, NMB kuendeleza vipaji kidigitali

TAASISI ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela na Benki ya NMB zimesaini mkataba wa hati ya mashirikiano unalolenga kutambua, kuhatamia na kuendeleza vipaji katika teknolojia za kidigitali.

Makubaliano hayo ya miaka mitano, yamesainiwa katika taasisi hiyo, Kampasi ya Tengeru Arusha, ambapo NMB imewakilishwa Ofisa Mkuu wa Rasilimali Watu, Emmanuel Akonaay.

Makamu Mkuu wa taasisi Profesa Maulilio Kipanyula akizungumza katika hafla hiyo, amesema sehemu ya makubaliano ni pamoja na namna ambavyo taasisi hiyo itashirikiana na NMB katika kutafuta rasilimali fedha kwa pamoja kkuendeleza matokeo ya utafiti na bunifu zinazozalishwa na wanataaluma na wanafunzi ili kuweza kufikia jamii na viwanda.

Amesema makubaliano hayo pia ni kuitumia Benki ya NMB kama sehemu ya kufanya mafunzo kwa vitendo kwa kupeleka wanafunzi kwa ajili ya kupata uzoefu ili kujua kinachoendelea katika jamii.

Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa NMB, Emmanuel Akonaay amesema, makubaliano hayo yanalenga kukuza uwezo wa teknolojia na kuweka mustakabali chanya wa watanzania katika teknolojia kupitia taasisi hizo, kwa kuweka misingi imara kwenye ukuaji wa teknolojia nchini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button