Taasisi yaguswa uzinduzi Daraja la JP Magufuli

TAASISI ya Mtetezi wa Mama, imesema Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mwenye dhamira ya kweli ya kuiletea maendeleo Tanzania, huku ikiwaomba wananchi kuhakikisha inampigia kura za kishindo katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza mara baada ya Rais Samia kuzindua Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi), Mkurugenzi wa Taasisi ya Mtetezi wa Mama, Neema Karume amesema tangu ashike usukani wa kuliongoza Taifa , Rais Samia amefanya mambo makubwa na yenye kuacha alama.

Amesema ukiacha ujenzi wa barabara, madaraja, upatikanaji wa huduma za maji , elimu, afya inayoenda sambamba na ujenzi wa hospitali pamoja na vituo vya afya, Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Tanzania inapaa kiuchumi huku akiimarisha diplomasia na mataifa mengine.

“Kuzinduliwa kwa Daraja la Kigongo- Busisi ambalo limegharimu kiasi cha zaidi ya Sh Bilioni 700, ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato Dodoma na miundombinu mingine iliyokamilika na inayoendelea na ujenzi inaonesha dhamira ya kweli ya kiongozi wetu kwa sisi wananchi wake,” amesema Neema.

Amesema Rais Samia ni kiongozi mwenye upendo kwa wananchi wake akisimamia kikamilifu ajenda ya kumtua mama ndoo kichwani pamoja na usambazaji nishati safi ya kupikia, jambo lililosaidia utunzaji wa mazingira.

“Naomba niwasihi Watanzania wenzangu kuhakikisha tunajitokeza kwa wingi katika uchaguzi Mkuu Oktoba na kumpigia kura nyingi, ili aweze kupata ushindi wa kishindo, hakika anastahili kupewa heshima hiyo kwa mambo mengi na mazuri aliyoyafanya,” amesisitiza Neema

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button