TACA yajipanga kuibua vipaji

CHAMA cha Makocha wa Riadha Tanzania (TACA) kimeandaa kozi ya awali kwa walimu wa mchezo huo itakayofanyika kuanzia Aprili 22- 27, Dar es Salaam.

Akizungumzia kozi hiyo, Charles Msengi Mmbaga ambaye ni Katibu Mkuu Chama Cha Makocha wa Riadha Tanzania(TACA) amesema wanatarajia kuwa na makocha 400 kuutoka Kanda ya Mashariki na maeneo mengine ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Amesema wameandaa kozi hiyo ya awali ya makocha ambayo itaendeshwa kwa siku sita chini ya wakufunzi wabobevu wa riadha kitaifa na kimataifa.

Amewataja wakufunzi hao kuwa ni Suleiman Nyambui (Chief Coach & International Coach ) Charles Maguzu kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na ni Mkufunzi wa Shirikisho la Riadha Duniani ( World Athletics( WA), Moris Okinda ambaye ni bingwa Taifa Mbio za Kuruka Vihunzi.

“Kozi hiyo imelenga kuwajengea uwezo walimu wote wa riadha hapa nchini ili wawe na uwanja mpana katika kugundua na kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi kuanzia shule za msingi mpaka sekondari, hivyo TACA tumepanga kufanya mafunzo hayo ili kupata watalaam wengi hapa nchini watakaoshirikiana na wadau mbalimbali wa mchezo wa riadha katika maeneo mbalimbali,”amesema Mmbaga.

Amesema TACA inawakaribisha walimu wote wa mchezo huu wa riadha waje kupata uzoefu kupitia kwa viongozi mbali mbali wa Riadha wenye utaalamu na wazoefu ambao watakuwepo kutoa uzoefu na mwongozo wa Makocha kuendeleza na kuinua viwango vya wachezaji chipukizi.

“Tunatumaini kuwa baada ya kozi hii waalimu watakuwa chachu katika kuibua vipaji vya vijana ambavyo vipo na vimejificha shuleni kwani kufanya hiyo ni katika kulisaidia taifa kuwa na wanamichezo mahiri ambao wamefundishwa kitaalamu kuanzia ngazi ya chin,”ameongeza Mmbaga.

Amewasihi waalimu kutumia fursa iliyopo mbele katika kujitokeza kupata mafunzo hayo yatakayowajenga na kuwa imara zaidi katika mchezo wa riadha kwani yatatolewa kwa nadharia na vitendo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button