Takukuru kutafiti akili bandia mifumo manunuzi

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inafanya utafiti wa kutumia akili bandia ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika mifumo ya ununuzi na michakato ya ufuatiliaji kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Mtafiti kutoka Takukuru, Manyama Venancy ameeleza hayo na kusema lengo la kutumia akili bandia ni kwa kuwa kumekuwa na tatizo kubwa la rushwa nchini.

Ameeleza zaidi kuwa,”Tulibuni kufanya uchunguzi wa akili bandia kuongeza uwezo na uwajibikaji katika mifumo ya ununuzi na michakato ya ufuatiliaji kwa kutumia teknolojia ya kisasa tutaweza kufanya utafiti wa mfumo ambao utapatia takukuru viashiria kwa kutokea kwa rushwa,”.

Amesema viashiria hivyo vya rushwa vitakapoonekana takukuru itaingilia huo mchakato ili kuzuia hali hiyo.

“Tunatarajia mchakato ukikamilika uwazi na uwajibikaji utaongezeka pia itapunguza rushwa, ikiwa ni pamoja na kupata maendeleo yaliyokusudiwa kwa wakati,” amesema.

Awali amesema kumekuwa na tatizo kubwa la rushwa katika nchi zinazoendelea, hapa nchini kuna shida kwenye manunuzi ya umma hasa katika miradi ya maendeleo kulingana na taarifa ya International Transparent inaonyesha;

“Karibu asilimia 20 ya bajeti iliyowekwa katika miradi ya maendeleo huwa inapotea kutokana na vitendo vya rushwa katika mifumo au michakato ya manunuzi,” amesema.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo alinukuliwa kusema kuwa utafiti na ubunifu umechangia kutatua changamoto mbalimbali  katika jamii ya watanzania.

Na kwamba uwekezaji wa serikali na wadau wengine katika utafiti nchini umewezesha kupatikana ufumbuzi wa changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa mbegu bora za mimea, mbolea, viuatilifu asilia na chanjo za magonjwa ya mifugo.

Alisema hali hiyo imesababisha serikali kuendelea kuongeza rasiliamali fedha kuweka mazingira rafiki na wezeshi ili  kuvutia wadau wengine ndani na nje ya nchi kuwekeza katika utafiti na ubunifu.

Habari Zifananazo

Back to top button