Takukuru Mtwara yaokoa mil 15/- AMCOSS

MTWARA: TAASISI ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mtwara imedhibiti upotevu wa zaidi ya Sh milioni 15.3 katika vyama vya msingi vya ushirika AMCOSS mkoani humo.

Akizungumza mkoani Mtwara leo Machi 3, 2026, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU, Mkoa wa Mtwara Mwanakombo Rajab amesema upotevu huo umeokolewa katika Wilaya ya Masasi, Tandahimba na Newala mkoani humo  katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2025.

Amefafanua zaidi kuhusu potevu huo kuwa, katika Wilaya ya Masasi kiasi cha fedha kilichodhibitiwa ni Sh milioni 11.8, Tandahimba Sh milioni 2.5 pamoja na Newala 800,000.

Mbali na hilo katika ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo taasisi hiyo imetoa mapendekezo ya kurekebisha mapungufu kwenye miradi nane yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 2 ikiwemo ya afya, elimu na mingine.

“Mapungufu hayo yamerebishwa kikamilifu baada ya kutembelea tena miradi hiyo na miundombinu imeanza kutoa huduma kwa wananchi,”amesema Mwanakombo

Pia taasisi hiyo imeendelea kutekeleza jukumu la uelimishaji wa umma ikiwemo uendeshaji wa semina 69 kwa wanafunzi wa vyuo wapatao 1,290 na kuimarisha klabu za wapinga rushwa 46 katika shule za msingi na sekondari mkoani humo.

“Tunaendelea kutekeleza jukumu la uelimishaji wa umma kwa kuendesha  semina 69 kwa wanafunzi wa vyuo wapatao 1,290 na kuimarisha klabu za wapinga rushwa 46 katika shule za msingi na sekondari kwenye mkoa wa mtwara,”amesema Mwanakombo

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button