MKUU wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Onesmo Buswelu, ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), wilayani humo, kufuatilia kwa ukaribu miradi ya madarasa ya shule za sekondari, ili kuhakikisha hautokei ubadhirifu wa aina yoyote.
Ameyasema hayo leo Oktoba 11, 2022 katika uzinduzi wa ujenzi wa miradi ya vyumba 9 vya madarasa kwa shule za sekondari, uliofanyika Shule ya Sekondari Kabungu na kueleza hatakuwa tayari kuona fedha za miradi hiyo zinapotea kwa namna yoyote ile.
Pia amezitaka Kamati za ujenzi, mapokezi na ununuzi za miradi ya madarasa ya shule za sekondari, kuhakikisha kwamba wanafanya kazi kwa kuzingatia kanuni na sheria zilizowekwabila kupindisha.
–